








Tanzania imeondokewa na nguli mwingine wa muziki wa dansi mwenye asili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo. Nguli huyu ni Kasaloo Kyanga aliyefariki dunia kwa tatizo la mapafu kujaa maji. Kasaloo alikuwa mahiri katika uimbaji na utunzi nyimbo zilizoshika chati ya juu katika muziki wa dansi Tanzania. Gwiji huyu alipitia bendi mbali mbali kubwa nchini ikiwemo Matimila, Tomatoma, Tancut Almasi, Marquiz original, Sambulumaa, Ngorongoro heroes na mpaka alifanikiwa kumiliki kundi lake aliloliita karubandika jazz band lililoasisiwa kule mombasa nchini Kenya mpaka likahamishia makazi yake hapa tena jijini Dar es Salaam. Marehemu ameacha mke na watoto. Safu hii na uongozi wake tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi. Maiti yake itazikwa kesho katika makaburi ya sinza alipozikwa gwiji mwingine hivi karibuni katika tasnia ya muziki wa dansi Dk.Remmy Ongala. Pichani anaonekana akiwa na baba wa CEO wa safu hii Mr. Kasambula Snr. enzi za ujana wao!
Wasalaam,
0 comments:
Post a Comment